Athari za ukataji misaada USAIDkwa afya ya uzazi kwa vijana
Dar es Salaam. Kama ulidhani kusitishwa kwa misaada ya maendeleo nje ya Marekani kulikofanywa na Rais wa nchi hiyo, Donald Trump kunawagusa wafanyakazi na walio mstari wa mbele pekee, umekosea.
Kukosekana kwa misaada hiyo kunawaamsha wadau, wanaobanisha kuwa litazidi kuongezeka la maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi, magonjwa ya zinaa, mimba za utotoni na vifo vitokanavyo na uzazi.
Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) lilikuwa na mnyororo mrefu katika kushughulikia afya, hasa afya ya uzazi ambapo vijana na vijana balehe zaidi ya milioni 21.3 nchini walinufaika kwa namna moja au nyingine.
Elimu kuhusu afya ya uzazi iliwafikia vijana moja kwa moja kupitia miradi mbalimbali, ikiwemo Dreams iliyosaidia vijana zaidi ya 70,000 nchini na Sharp Project ambayo iliwafikia maelfu ya vijana katika mikoa ya Dodoma, Morogoro na Manyara.